Kuna kila dalili kuwa Beyoncé yupo mguu nje ndani kwakuwa anadaiwa kwenda kusaka nyumba ya kununua bila kumshrikisha Jay Z, vyanzo vimeliambia gazeti la New York Post.
Mrembo huyo alienda kuangalia nyumba yenye thamani ya dola milioni 21.5 huko Chelsea mapema mwezi uliopita – wiki chache baada ya video inayoonesha mdogo wake Solange Knowles akigombana na Jay kwenye lifti.
“Alikuwa mkimya sana kama vile alikuwa anajificha,” kilisema chanzo. Chanzo hicho kimesema mara zote Jay Z huhusika kwa kiasi kikubwa katika utafutaji wa nyumba na hivyo huenda Beyoncé anatafuta nyumba yake mwenyewe atakayoishi na mwanae Blue Ivy.
Post a Comment