Mipango ya usajili ya klabu ya Southampton yanaswa na Daily Mail




















Siri nzito ya meneja wa klabu ya Southampton Ronald Koeman ya nani atakaemsajili mwishoni mwa juma hili imeanza kufichuka, kufutia baadhi ya vyombo vya habari kutambua mipango aliyojiwekea.
Muandishi wa gazeti la Daily Mail, John Drayton amebaini mpango wa
meneja huyo kutoka nchini Uholanzi wa kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Mexico na klabu ya Man utd, Javier Hernandez.

Koeman, anajipanga kufanikisha mpango huo, huku akiwa tayari kupambana na viongozi wa Inter Milan ambao wameonyesha nia ya kuinasa saini ya mshambuliaji huyo.
Inadaiwa kuwa Koeman amejipanga kuwasilisha ofa nzito ambayo itakuwa ni zaidi ya Inter Milan kwa ajili ya kumnasa kirahisi Chicharito ambaye kwa sasa yupo kambini nchini Marekani sambamba na wachezaji wengine wa klabu ya Man Utd.
Chicharito yupo kwenye mipango ya kuuzwa na Man Utd, kufuatia kutokuwepo katika mikakati ya meneja wa sasa Louis Van Gaal ambaye anaonekana kumtumia zaidi Wayne Mark Rooney pamoja na Danny Welbeck.

Www.theheadliner24hrs.blogspot.com




Post a Comment

Previous Post Next Post