WANANDOA WA KANADA WANAO HUSIKA WIZI WA SIRI ZA NCHI KUFANYIWA UCHUNGUZI CHINA.

Wanandoa wa Canada kuchunguzwa China


Rais wa China Xi Jinping

Mamlaka za China zinawatuhumu wana ndoa raia wa Canada wanaofanya biashara ya mgahawa nchini kwamba wanahusika na wizi wa siri za nchi kuhusiana na masuala ya utafiti wa kijeshi.
Wanandoa hao wanamiliki mgahawa wao katika mji wa Dangdong karibu na mpaka wa Korea Kaskazini.

Kevin na Julia kwa sasa wanafanyiwa uchunguzi na idara za usalama Kaskazini Mashariki mwa Dandong. Mgahawa Kevin na Julia umekuwa maarufu kwa watalii na raia wengine wa China hasa wale wanataka kujifunza kiingereza.

Haijafahamika mara moja ni kwa jinsi gani wanandoa hawa wamekuwa wakiiba siri za nchi, ingawa mtandao wa umekuwa ukiwasaidia wageni kuvuka mpaka kwenda Korea Kaskazini.
Nchini China makosa ya wizi ya taarifa za serikali ni adimu kutokea, japo kuwa makosa yaliyo mengi nchini humo hukumu yake huwa ni kifo.
 BBC swahili inahabarisha
Www.theheadliner24hrs.blogspot.com

Post a Comment

Previous Post Next Post