ARTURD VIDAL APATA MAJERAHA YA GOTI AKIWA NA LA ROJA (THE RED ONE)


Meneja wa klabu ya Man Utd, Louis van Gaal huenda alikuwa sahihi kuachana na mipango ya kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji kutoka nchini Chile pamoja na klabu bingwa nchini Italia Juventus, Arturo Erasmo Vidal Pardo.


Jibu la maamuzi aliyoyachukuwa van Gaal, limepatikana baada ya kubainika Vidal, anakabiliwa na mtatizo ya goti ambayo huenda yakamchukuwa muda mrefu zaidi kurejea tena uwanjani na kuitumikia klabu ya Juventus katika msimu huu wa ligi huko nchini Italia.


Man Utd walikuwa wameshatenga kiasi cha paund milio 42 kwa ajili ya kukamilisha mpango wa kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, na walikaribia kutimiza lengo lakini dakika za mwisho mambo yalikwenda ndivyo sivyo.


Endapo mpango huo ungefanikiwa, huenda Man utd wangekuwa wameingia kwenye hasara ya kumsajili mchezaji mgonjwa ambaye asingeweza kukamilisha azma ya meneja Louis van Gaal aliye na uchu wa kuipa mafanikio klabu hiyo ya Old Trafford.


Taarifa kutoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Chile zinaeleza kwamba Vidal ameumia goti akiwa kwenye mazoezi ya timu hiyo ambayo katika kipindi hiki cha majuma mawili itakuwa inakabiliwa na mchezo ya kimataifa ya kirafiki.


Lakini taarifa hizo hazijaeleza jeraha la Vidal lina ukubwa kisi gani, hali ambayo inaendelea kuzua hofu kwa mashabiki wa Juventus ambao wanaamini msimu huu watamshuhudia mshambuliaji huyo akiendelea kuonyesha makali yake.

No comments

Powered by Blogger.