BAVICHA LATOA TAMKO KUFUATIA MAUAJI YA KIKATILI YA KIJANA ALIYEKUA MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA GEITA
Baraza la taifa la vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema (Bavicha) limetoa tamko la kulaani vikali mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Geita Alphonce Mawazo na kumtaka rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dk. John Pombe Magufuli kutoa msimamo wa serikali kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu, utawala wa sheria na haki za kidemokrasia.
Mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema taifa Patrobas Katambi amesema vijana nchini wamechukizwa na matendo maovu ya utekaji, mauaji, uvamizi na mashambulio ya kimwili kwa makusudi, kamatakamata ya polisi na ubambikizwaji wa kesi za jinai kwa viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani unaoendelea nchini kote.
Aidha Bavicha imemtaka rais Dk. Magufuli na wakuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama kutoa agizo maalum la kushughulikia kwa haraka upelelezi wa kesi zote za mauaji yanayodaiwa kufanywa kinyama, yakiwemo ya aliyekuwa mjumbe wa tume ya katiba Dk. Sengodo Mvungi, mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam Prof. Juan Mwaikusa na aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha channel ten David Mwangosi.
No comments