HUYU NDIE WAZIRI MKUU WA TANZANIA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO, USHINDI WA KISHINDO WA KURA 258---->
Mh. Kassim Majaliwa amethibitishwa na wabunge kuwa Waziri Mkuu mteule kwa kupata kura za ndio 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote 351 zilizopigwa.
Kura za hapana ni kura 91 sawa na asimilia 25 ya kura zote, na kura zilizoharibika ni 2.
Majaliwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kumwamini na ameahidi kuwatumikia watanzania wote bila kujali itikadi zao za vyama.
No comments