KAMA ULIKUA HAUJAIPATA, HUYU NDIYE SPIKA WA BUNGE NA WABUNGE WATEULIWA WAMO HAPA----->>

Wakati jana wabunge wateule wakianza kujisajili kwa ajili ya kuanza vikao vya Bunge la 11 Jumanne wiki ijayo, pamoja na mambo mengine wameeleza sifa za spika ajaye katika bunge hilo ambalo linaundwa na vijana wengi tofauti na miaka iliyopita.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika viwanja vya bunge mjini hapa wakati wa kufanya usajili, baadhi ya wabunge waliopata fursa hiyo, walisema bunge la sasa ni gumu tofauti na bunge lililopita kutokana na kuwapo kwa wabunge wengi wenye upeo mkubwa na vijana.
Wengi walisema moja ya sifa anazotakiwa kuwa nazo spika ajaye ni kumudu kuendana na kasi ya wabunge na kutopendelea upande wowote.
Dk. Kigwangala
Mbunge mteule wa Nzega Vijijini, Dk. Hamisi Kigwangala (CCM), alisema matarajio yake kwa spika ajaye, anatakiwa kuwa na hekima kutokana na kuwapo kwa ushindani ndani ya bunge.
“Mimi natarajia apatikane spika ambaye atakuwa na hekima, kwani bunge la safari hii litakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kuongezeka wabunge mahiri na wenye upeo mpana,”alisema Dk. Kigwangala.
Alisema ni lazima apatikane spika ambaye ataendana na kasi ya wabunge na Rais Dk. John Magufuli.
Hata hivyo, alisema katika azma ya kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi, ni vema rais akachagua sura mpya katika baraza lake la mawaziri badala ya kuwa na sura zinazojirudia kila wakati.
“Wananchi wameonesha imani kubwa kwa rais kwamba atamaliza ule mfumo wa kuchagua sura za mawaziri zile zile,”alisema mbunge huyo. Aidha, alisema wananchi kwa sasa wamebadilika na wanataka mabadiliko ndiyo maana katika uchaguzi wa mwaka huu  kulikuwa na ushindi mkubwa.
“Ni vema akachagua sura mpya kabisa ambazo zitawafanya wananchi kulikubali na kuamini, hivi sasa wananchi wanaamini kuwa bila mabadiliko katika Baraza la Mawaziri hususan kwa kuleta sura mpya kuna uwezekano baada ya miaka mitano hali ya kimaendeleo ikabaki hivi hivi, “alisema Dk. Kigwangala.
MCHUNGAJI MSIGWA
Kwa upande wa Mbunge mteule wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema), alisema anashukuru kurejea bungeni na kudai kuwa uchaguzi wa mwaka huu ulikuwa mgumu na kufananisha na vita huku akidai kuwa haukuwa wa kidemokrasia.
“Uchaguzi ulivyoendeshwa ni kinyume cha demokrasia, katika bunge hili tutahakikisha tunaendelea kuibana serikali ipatikane Tume Huru ya Uchaguzi, Katiba mpya, kupambana na ufisadi na wizi wa fedha za umma,”alisema Msigwa.
Alisema anatarajia kuona akipatikana spika kijana ambaye atakuwa na maono na hatafungamana na itikadi zozote za kisiasa.
Alisema anaamini akipatikana spika kijana, atakuwa na weledi mzuri katika kuendesha bunge bila kuwapo kwa upendeleo wowote.
“Spika awe kijana, asiwe anatoka kwenye mfuko wa chama chochote cha siasa,  ukipata spika ambaye anaushabiki, tutaishia kuona bunge la chama kimoja,”alisema Msigwa.
Ahmed Shabiby
Mbunge mteule wa Jimbo la Gairo, Ahmed Shabiby (CCM), alisema anatakiwa spika ambaye ataweza kukabiliana na changamoto za kibunge kutokana na kuwapo na vijana wengi wenye upeo mpana.
Alisema spika anayetakiwa kuongoza bunge, lazima awe makini na mchapakazi.
LUSINDE
Naye Mbunge mteule wa Jimbo la Mtera, Livingstone Lusinde (CCM), alisema anatakiwa spika ambaye atatokana na wabunge na si nje ya wabunge.
“Tunahitaji wenye uzoefu kama vile awe amewahi kuwa mwenyekiti au naibu spika maana atakuwa na uzoefu wa kutosha, na ukisema hivyo maana katika wote waliojitokeza wenye sifa ni wawili tu,”alisema Lusinde.
Ngonyani
Kwa upande wake, Mbunge mteule wa Korogwe Vijijini(CCM), Stephen Ngonyani, alisema kutokana na bunge la safari hii kuwa la tofauti, ni vema akapatikana spika ambaye ataendana na kasi ya wabunge sambamba na kasi ya rais.
“Hivi sasa tuna kazi kubwa  ya kufanya kwa sababu Watanzania wa juzi si wa sasa, hawataki kuchoshwa na mambo ambayo hayatekelezeki,” alisema Ngonyani.
profesa j
Naye Mbunge mteule wa Mikumi, Joseph Haule maarufu kwa jina la Profesa J (Chadema), alisema anatarajia kuona akipatikana spika ambaye atakuwa mzalendo na atakayesimamia mshikamano na umoja.
Alisema sifa kubwa ya spika ambaye anatakiwa kwa sasa, ni lazima awe mzalendo na ambaye atatenda haki.
Hata hivyo, alisema wabunge wana kazi kubwa kuhakikisha wanakabiliana na changamoto ambazo zilijitokeza ikiwamo katika mchakato wa katiba ambao alidai kuwa maoni ya wananchi hayakuwapo.
Pauline Gekul
Mbunge mteule wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul (Chadema), alisema bunge hilo litakuwa la moto na kwamba dharau za wazi wazi hazitakuwapo.
“Kutokana na wabunge wa upinzani kuongezeka bungeni, kutakuwa na mpambano mkali sana, hivyo apatikane spika ambaye hatapendelea chama chochote,”alisema Gekul.Wakati jana wabunge wateule wakianza kujisajili kwa ajili ya kuanza vikao vya Bunge la 11 Jumanne wiki ijayo, pamoja na mambo mengine wameeleza sifa za spika ajaye katika bunge hilo ambalo linaundwa na vijana wengi tofauti na miaka iliyopita.

“Kutokana na wabunge wa upinzani kuongezeka bungeni, kutakuwa na mpambano mkali sana, hivyo apatikane spika ambaye hatapendelea chama chochote,”alisema Gekul.

No comments

Powered by Blogger.