MAALIM SEIF AKINUKISHA WINGEREZA, WAANDAMANA WAKISHINIKIZA ATANGAZWE MSHINDI
Maandamano hayo yaliandaliwa na Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association (ZAWA) ambapo wazanzibari hao walitoka maeneo mbali mbali katika miji yao na kukusanyika katika eneon la Downing Street kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na uongozi huo kukabidhi barua yao yenye malalamiko kutaka suala la Zanzibar lishughulikiwe.
Maandamano hayo yalifanyika kwa lengo la kuongeza shindikizo kwa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua hatua za haraka ya kuhakikisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inakamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Zanzibar iliingia katika mkwamo wa kisiasa baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha Octoba 28 kutangaza kuufuta uchaguzi wote kwa madai kwamba ulikumbwa na matatizo mbali mbali.
Wakati jecha akitoa tangazo la kufuta matokeo bila ya kushauriana na tume yake alikuwa tayari ameshatangaza matokeo ya kura za urais za majimbo 31 kati ya 54 ya Zanzibar pia washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani katika majimbo hayo walishatangazwa na walishakabidhiwa vyeti vyao.
Rashid Ali ambaye ni kiongozi wa ZAWA alisema jana kuwa wamewasilishwa barua hiyo wakiamini kwamba suala la Zanzibar litashughulikiwa ili wananchi wa Zanzibar waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Mwakilishi wa ZAWA, Hassan Khamis alisema wameamua kupeleka barua kwenye ofisi za waziri Mkuu wakiamini suala hilo litashughulikiwa ikiwa ni pamoja na serikali ya Tanzania kuchukua hatua madhubuti na za haraka kaika kushughulikia suala hilo ambalo limewaweka wazanzibari roho juu.
No comments