LOWASA AELEZA ATAKACHOKIFANYA ENDAPOATATANGAZWA AMESHINDWA KATIKA UCHAGUZI MKUU OCTOBER 2015

ZIKIWA  zimebakia  siku 30  kabla  watanzania  hawajapiga  kura  ya  kumchagua  Rais,mgombea  urais  kwa  tiketi  ya  CHADEMA, Edward  Lowassa  ambaye  amekuwa  akieleza  imani  yake  kuwa  atashinda  kwa  kishindo, ameeleza  msimamo  wake  endapo  tume  ya  Taifa  ya  Uchaguzi  itatangaza  matokeo  tofauti  na  ya  matarajio  yake.

Akiongea  na  kituo  cha  Runinga  cha  Citizen  cha  nchini  Kenya, Lowassa  amesema  hawezi  kusema  kama  atakubali  au  atakataa  hadi  itakapothibitika  kuwa  matokeo  hayo  hayajahujumiwa.

"Siwezi  sema  nitakuchukulia  kama  nimeshindwa  hadi  nitakapothibitishiwa  kuwa  kila  kitu  kimeenda  sawa  na kwamba  hakuna  hujuma." Alisema  Lowassa  na  kuongeza;

"Tunaogopa  sana  kuhusu  hujuma.Kila  mtu  unayeongea  naye  unapokutana  naye, anakwambia  utashinda, lakini  je, watakubali  kushindwa?"

Katika  hatua  nyingine,Lowassa  alijibu  swali  la  mwandishi  lililomtaka  kueleza  kama  angeweza  kusema  anachokisema  hivi  sasa  kuhusu  CCM  endapo  angechaguliwa  kuwa  mgombea  Urais  kwa  tiketi  ya  CCM.

"Ninasema  vitu  vingi  ambavyo  vingeweza  kufanywa  vizuri  zaidi  na  CCM,na  ninasema  vitu  vingi  ambavyo    ninaweza  kuvifanya  vizuri  zaidi  nikiwa  Upinzani."  alisema  Lowassa.

No comments

Powered by Blogger.