DIAMOND AZUA HAYA KWENYE KAMPENI ZA MAGUFULI.

Kundi kubwa la vijana wakigombea kumuona mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’, katika Viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba.
Stori: Richard Bukos aliyekuwa Kagera
UNAZI! Kundi kubwa la vijana wa kike na kiume, mwanzoni mwa wiki iliyopita walizua kizaazaa baada ya kumgombea kumuona kwa karibu na kutaka kuzungumza na mkali wa muziki wa Kizazi Kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ mara baada ya kumaliza kutumbuiza katika mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli uliofanyika katika Viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba.
Baunsa wa Diamond akiwatoa vijana na akina mama waliolizonga gari alimokuwa Diamond.
Baada ya kumaliza ngwe yake ya kuburudisha, msanii huyo aliteremka jukwaani na kwenda alikopangiwa kukaa, lakini alifuatwa na dada mmoja aliyetaka kuzungumza naye, huku vijana wengine wakisogea eneo hilo, kitu ambacho mabaunsa walikikataa na kumfanya msanii huyo kukimbilia katika basi dogo aina ya Coaster lililokuwa limetayarishwa kwa ajili yake na wacheza shoo wake.


…Wakilikimbilia gari hilo baada ya kuondoka viwanjani hapo.
Hata hivyo, wakati mkutano huo ukiendelea, umati zaidi wa vijana uliendelea kulifuata basi hilo na kujazana katika dirisha alilokaa Diamond, jambo lililowapa wakati mgumu mabaunsa kuwasogeza, hadi polisi walipofika na kufanikiwa kuwatawanya, huku gari hilo likiondolewa eneo hilo.
Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.
Hata hivyo, baada ya basi hilo kupata upenyo wa kumkimbiza mwanamuziki huyo, kundi kubwa la vijana wa kike na kiume walilifukuza gari hilo mpaka dereva alipoongeza kasi.

Kabla ya mkutano huo mkoani hapa, Magufuli alianza kunadi sera zake katika Vijiji vya Kaziramuyagwa, Kyamyorwa, Kasharunga, Rulanda na kufanya mkutano mkubwa katika Uwanja wa Zimbihile uliopo Muleba Kusini jimbo analogombea Prof. Anna Tibaijuka.
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Baada ya hapo kampeni zilihamia Muleba Kaskazini ambapo Magufuli alimwaga sera katika maeneo ya viwanja vya wazi vya Kamachumu, Maruku na Jimbo la Bukoba vijijini kabla ya kufanya mkutano wa kihistoria katika viwanja vya Bukoba mjini.

No comments

Powered by Blogger.