WABEBA TV ZAO NA KUZIPELEKA BUNGENI.
Katika hali ya kushangaza wananchi wa Uganda jana walibeba televisheni zao na kuzipeleka bungeni kupinga kitendo cha serikali kuamulisha kufungwa kwa mfumo wa analog waliozoea na kuelekezea kwenye mfumo wa digital wakati wananchi hawajapewa elimu ya kutosha kuhusiana na mfumo huo.
Hatua hiyo ilisababisha kuibuka kwa lawama nyingi ambazo zilielekezwa kwa serikali ya nchi hiyo kushindwa kuwatetea wananchi wake.
Kutokana na hali hiyo hakimu wa mahakama kuu Moses Ntende Kagoda jana alitoa amri ya kurudishwa mara moja mfumo huo wa zamani (Analog) ili kuepusha tafrani kutoka kwa wananchi.
No comments