KABURI LA BALALI KUFUKULIWA BAADA YA MABISHANO YA MDA MREFU
HII mpya! Kuna
madai kwamba, kaburi la aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), marehemu Daudi Timoth Ballali lililopo Makaburi ya Gate of Haeven
(Geti la Mbinguni) Eneo Na. 6, Ploti Na. 241, Safu Na. 17 huko Maryland
nchini Marekani lipo mbioni kufukuliwa ili kuwezesha vipimo vya
vinasaba (DNA) kutumika kwa lengo la kubaini ukweli wa kifo chake,
Ijumaa limeelezwa.
Gharama
ya jumla ya kuwepo kwa kaburi hilo ambalo safu yake imepewa jina la
Jesus In The Temple (Yesu Hekaluni) ni Dola za Marekani 4,800 (zaidi ya
Sh. milioni 9 za Tanzania).Kwa mujibu wa ndugu mmoja wa Ballali
aishiye Bongo, familia inaona ni vema kutimizwa kwa ombi hilo kwa vile
manenomaneno kuhusu ‘Ballali kafa au hajafa?’ hayajawahi kufunga breki
tangu tangazo la kifo chake, Mei, mwaka 2008.
TWENDE PAMOJA
“Nadhani sisi
familia hatuna umoja. Wengine waoga, wengine majasiri. Lakini kwa sababu
hata sisi hatukuwahi kwenda Marekani kumzika ndugu yetu (Ballali),
hivyo ili na sisi tuwe na amani na kujua moja, tumetoa wito kwa serikali
ya Tanzania kuwasiliana na Marekani kwa lengo la kulifukua kaburi lake
na kuutoa mwili.
Edward Lowassa.
“Hilo ni moja.
Pili, mwili huo upimwe DNA ili kubaini kama aliyezikwa ni Ballali? Hili
zoezi halitatusaidia sisi tu kama familia, lakini hata serikali yenyewe
itakuwa na faida maana maneno yamekuwa mengi sana. Tumeshaandaa
utaratibu wa kuonana na serikali kwa ajili ya kupanga hili,” alisema
ndugu huyo akisisitiza kusitiriwa kwa jina lake.
BALLALI FEKI AUMIZA KICHWA
Ndugu huyo
aliendelea kusema kuwa, tangu kifo cha Ballali, Mei, mwaka huo, Desemba
posti ya kwanza ya mtu aliyejiita Ballali ilitupiwa kwenye mitandao ya
kijamii akisema amekumbuka nyumbani Tanzania.
“Tangu wakati
huo, mtu huyo amekuwa akitupia maneno ya kushutumu kwamba yeye amefariki
dunia. Hata vyombo vya habari vya Tanzania vilipotembelea Marekani
mwaka jana na kuthibitisha kifo cha mchumi huyo kwa kuliona kaburi lake,
mtu huyo alisema anavishangaa vyombo hivyo kwa vile yeye yu hai.“Ndiyo
maana tunataka kaburi kufukuliwa, mwili utolewe na kufanyiwa vipimo mara
moja ili kuondoa utata huu,” alidai ndugu huyo.
WATOTO WA BALLALI KUTUA BONGO
Benard Membe.
Ndugu
huyo alizidi kuweka bayana kuwa, habari alizonazo ni kwamba, watoto
wawili wa marehemu ambao alizaa na mwanamke, raia wa Marekani wapo
kwenye mchakato wa kutua Bongo wakati wowote kwa mambo mawili makuu.
“Nasikia wanakuja. Lakini lengo la
ujio wao ni kusema wanachokifahamu kuhusu kifo cha baba yao. Sasa
sijajua watasema alifariki dunia au hajafariki dunia! Hiyo ni siri yao
nzito, ipo mioyoni mwao.
“Lakini
nijuavyo mimi kilio kikubwa cha hawa watoto mwaka ule wa tangazo la kifo
kilikuwa ni kukosa kuiona sura ya baba yao wakati wa kuuaga mwili mpaka
unaingizwa kaburini kwa mazishi.
“Kingine
wanafuatilia hisa. Baba yao aliweka hisa kiasi cha shilingi bilioni 3
kwenye kampuni moja ya bia Tanzania. Sasa kutokana na kusuasua kwa
maelezo yasiyonyooka kuhusu faida na hasara za hisa zile, ndiyo maana
wanakuja. Nasikia tayari wana mwanasheria kwa ajili ya kupata haki yao
hiyo,” kilimalizia chanzo hicho.
LOWASSA AOMBWA KUMLETA BALLALI
Katika Kampeni
za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu, mgombea wa urais kwa ‘leseni’
ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia mwavuli wa Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa amekuwa akiombwa na
wapiga kura wake kumleta Ballali mara tu atakapoingia ikulu, jambo
ambalo alikubaliana nalo.
Lakini naye
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe
ameibuka na kuonesha kushangazwa na suala hilo kwani anachokijua kama
waziri mwenye dhamana ni kwamba Ballali alifariki dunia mwaka 2008
SOURCE: UDAKU SPECIA.
Udaku special Source:Global Publishers
YAP!, DUNIA HAINA SIRI.
ReplyDelete