GAUDENCE MWAIKAMBA: SIAMINI USHIRIKINA KWENYE SOKA
Ushirikina ni jambo ambalo limekuwa likihusishwa kwa kiasi kikubwa katika soka hususani barani Afrika, hata katika timu zetu za Ligi Kuu Tanzania bara zimekuwa zikifanya baadhi ya vitu ambavyo vinahusishwa na imani za kishirikina, millardayo.com ilipata bahati ya kufanya exclusive interview na Gaudence Mwaikimba kuhusu ishu za ushirikina katika soka.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Gaudence Mwaikimba ni mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Dar Es Salaam Young Afrika, Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Mwaikimba kwa sasa anachezea klabu ya JKT Ruvu ila ni kweli anaamini ushirikina katika soka yeye kama mchezaji mkongwe?
Mwaikimba amekiri katika soka kuwa na imani za kishirikina ila yeye haamini kama inaweza msaidia mtu kucheza vizuri au kufunga magoli katika mechi, ila amewahi kushuhudia mtu akianguka uwanjani baada ya kuingia na irizi ila baadae alianguka na kuanza kutoa mapovu mdomoni.
“Ndio maana hadi leo mimi siamini ushirikina katika soka kwani nimewahi kushuhudia mtu akianguka uwanjani sababu ya hivyo vitu ila ilikuwa Ligi daraja la tatu, ilikuwa ni mtu kaweka irizi mguuni, mwisho wa siku akapigana kibuyu na mchezaji wa timu yetu akaanguka na kuanza kutoa povu kumvua soksi akakutwa na irizi”
No comments