Morrison alitibua tena Simba! Apost katika ukurasa wake wa instagram “Something huge about to BLOW” Guess what???????????

Morrison alitibua tena Simba!
Apanga kulipua bom...

UONGOZI wa klabu ya Simba, umemsimamisha kwa muda usiojulikana winga wao Bernard Morrison kutokana na matukio ya kujirudia rudia ya utovu wa nidhamu.

Morrison alisajiliwa Simba akitokea Yanga usajili uliozua sintofahamu kutokana na nyota huyo kudaiwa kuwa na mkataba na wanajangwani hao mpaka kesi hiyo kutinga CAS.

Taarifa ya Simba iliyotumwa leo Februari 4 jioni, imesema imefikia hatua hiyo baada ya mchezaji huyo matukio yake ya kinidhamu kujirudiarudia.Nyota huyo amekumbwa na mkasa huo baada ya kutoroka kambini kinyume na taratibu ambazo wachezaji wengine wanazifuata lakini yeye anakaidi.

"Mara ya mwisho Morrison alitoroka kambini na uongozi na benchi la ufundi ulimpa maelekezo kuwa asirejee kambini mpaka atakapoonana na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez,"Hata hivyo nyota huyo hakutii maagizo hayo hivyo kuendelea kukaa nje ya kambi.

"Kufuatia kadhia hiyo uongozi wa klabu umemsimamisha kwa muda na kumtaka atoe maelezo ya maandishi kwa mtendaji Mkuu na akishindwa kufanya hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake,"

Morrison anapata rungu kama ambalo walilipata nyota wa Azam FC Salum Abubakar 'Sure Boy', Aggrey Morris pamoja na Mudathir Yahya ambao nao walisimamishwa kwa muda usiojulikana kutokana na utovu wa nidhamu. Hataivyo ivyo Bernard Morson saa chahche zilzopita ametoka kupost picha akiwa na mabegi huku akisindikiza pich iyo na caption isemayo 


“Something huge about to BLOW”
Guess what???????????
"


credity; Mwananchi


No comments

Powered by Blogger.